Ligi Kuu Uingereza Leo ni 4-4-2

KIVUMBI cha ligi kuu nchini Uingereza kimeendelea leo kwa michezo mitatu ambapo matokeo ni kama mfumo wa uchezaji soka 4-4-2 huku Crystal Palace, Liverpool na Tottenham Hotspur wakiibuka na ushindi katika michezo yao.

Katika mchezo wa mapema Palace waliichimbia ‘kaburi’ Hull City inayoshika nafasi ya tatu toka mkiani kwa kuibamiza mabao 4-0 na kuiacha na pointi zake 34 katika mstari wa kushuka daraja.

Daniel-Sturridge-Liverpool-West-Ham-804478

Liverpool inayoshika nafasi ya tatu ikaibamiza West Ham United mabao 4-0 huku Philippe Coutinho akiibuka shujaa kwa kupachika mawili na kusaidia upatikanaji wa jingine moja lililofungwa na Daniel Sturridge.

Bao la nne la Liverpool katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki 56,985 kwenye dimba la London Stadium lilifungwa na Divock Origi dakika 14 kabla mwamuzi Neil Swarbrick hajapuliza kipenga cha mwisho.

2913

Katika mchezo uliomalizika hivi punde, Mashetani wekundu Manchester United wamekubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Spurs ambao walikuwa kwenye dimba la nyumbani White Hart Lane.

Victor Wanyama na Harry Kane waliifungia Spurs inayoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 80 huku lile la kufutia machozi la United likifungwa na Wyne Rooney wakibakia na pointi 65 katika nafasi ya sita.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *