LIPULI YAICHAKAZA SINGIDA SAMORA

Lipuli FC imeibuka na ushindi wa bao moja mbele ya Singida United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika katika uwanja Samora mkoani Iringa.

Tangu ilipoitoa Yanga katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya FA, Aprili mosi Singida imeshindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye michezo ya ligi.

Mshambuliaji Malimi Busungu ndiye alipeleka kilio kwa vijana hao wa kocha Hans van Pluijm baada ya kufunga bao hilo dakika ya 17.

Lipuli imefikisha pointi 31 ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wakati Singida ikibaki nafasi ya tano na alama zake 37.

Mchezo mwingine Stand United imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui FC wakati Mbao FC ikibanwa na mbavu na Majimaji kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *