LIPULI YAMKALIA KOONI AMRI SAID

Uongozi wa klabu ya Lipuli FC umesema hauna taarifa ya kuondoka kwa kocha wao mkuu Amri Said kwakua bado wana mkataba nae.

Wiki iliyopita Amri alitangazwa kuwa kocha mpya wa Mbao FC kitu ambacho kiliwashtua Wana Paluhengo hao na kutoa tamko kuwa bado mkataba wake haujamalizika.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ramadhan Mahano amesema kocha huyo amebakisha mkataba wa miezi miwili kama anataka kuondoka inabidi auvunje ili awalipe.

Amri said akitambulishwa na klabu ya Mbao mara baada ya kusaini kandarasi ya kuitumikia
“Tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa Amri ameondoka ila hajatuletea taarifa rasmi lakini anatakiwa afahamu bado amebakiwa na miezi miwili kwenye mkataba wake,” alisema Mahano.

Amri amechukua nafasi ya kocha Ettiene Ndayiragije aliyejiunga na timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) ambayo imepanda msimu huu.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *