LIVERPOOL KUIPIKU ARSENAL KWA LEMAR

Liverpool wanaongoza mbio za kumuwania winga wa AS Monaco, Thomas Lemar na kuzipiku timu za Arsenal na Chelsea ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya nyota huyo.

Majogoo hao walihitaji saini ya Mfaransa huyo majira ya joto yaliyopita lakini hawakuwa tayari kulipa dau la pauni 70 milioni ambalo Monaco walikuwa wanalitaka.

Arsenal walikubali kumsajili Lemar kwa pauni 90 milioni msimu uliopita lakini ikashindikana baada ya sintofahamu ya Alexis Sanchez kutaka kujiunga na Manchester City siku ya mwisho ya usajili.

Washika bunduki hao bado wanahitaji saini ya Lemar lakini Liverpool wana pesa nyingi mkononi baada ya kumuuza Phillipe Coutinho kwenda Barcelona wiki hii kitu ambacho kinawapa nafasi ya kumtwaa Mfaransa huyo.

Tayari Jurgen Kloop ametumia pauni 75 milioni kumsajili mlinzi Virgil Van Dijk kutoka Southampton katika dirisha hili la usajili ambapo anatarajia kutumia zaidi ya kiasi hicho.

Meneja wa Monaco, Leonardo Jardim amekiri mapema wiki hii kuwa Lemar ataondoka klabuni hapo mwezi huu kama kuna klabu itatoa dau la pauni 90 milioni.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *