Liverpool yazidi kuiwekea ‘msuli’ Barcelona

MERSEYSIDE, Uingereza
BAADA ya kumpoteza nyota wake Neymar Da Silva aliyejiunga na PSG kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia, Barcelona imekuwa ikitafuta mbadala wake ambapo kwa mara ya pili dau la paundi 90 milioni limekataliwa na Liverpool ili kumwachia Phillipe Coutinho.

Barcelona ina kiasi cha euro 222 milioni baada ya kumuuza Neymar ambapo hadi sasa wanajiuliza anayeweza kuchukua mikoba yake huku wakiweka nguvu nyingi kwa Coutinho ambaye Majogoo hao wa Anfield wamekataa kumuachia.

Kumekua na taarifa mbalimbali zikisema kuwa Barcelona ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa raia huyo wa Brazil, lakini Liverpool imekataa dau hilo ili kumruhusu kuelekea nchini Hispania.

Coutinho

Ni wazi Liverpool wanategemea kuvuna kiasi kikubwa cha pesa kwani wanajua Barcelona wanahitaji kutafuta mbadala wa Neymar huku wakiwa na fedha za kutosha.

Dili hili la Coutinho linategemea Liverpool zaidi kwani wanahitaji pesa ili kumnasa mshambuliaji Naby Keita kutoka RB Leipzig ya Ujerumani hivyo huenda wakasubiria dau kubwa zaidi ili kumpa Coutinho mkono wa kwaheri.

Mbali na Keita, Liverpool inataka kumsajili beki Virgil Van Dijk waliyemfukuzia kwa muda mrefu kutoka Southampton.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *