Lukaku ashindwa kung’aa, City ikiiadhibu Stoke,Crystal Palace wakifunga bao la kwanza ndani ya dakika 731.

Ilimchkua dakika 17 kwa Romelu Lukaku kugusa mpira tangu kipyenga kilipopulizwa kwenye mchezo ambao Manchester imeshindwa kuendeleza ubabe wake katika ligi kuu England kufuatia sare ya bila ya kufungana dhidi ya Liverpool katika mchezo uliopigwa Anfield jijini Liverpool.

Mlinda mlango wa United De gea, leo hii ameibuka shujaa baada ya kuchomoa mpira uliopigwa na Mkameruni Matip,uliokua unaelekea golini na kuwanyima Liverpool nafasi ya kuongoza mchezo huo.

De Gea akiokoa mpira uliokua ukielekea langoni.

Wakati miamba hiyo ikienda sare, Manchester city ikiongozwa na mwalimu bora wa mwezi wa 9, imeitandika Stoke city kwa jumla ya magoli 7 kwa 2.Mabao ya city yamefungwa na Gbriel Jesus (2) Raheem Sterling (1) David Silva (1) Fernandinho (1) Leroy Sane (1) na Bernado Silva. Ushindi huo umeifanya City kufikisha alama 22 na kuongoza msimamo wa ligi hyo.

Kiungo wa City Fernandinho akifunga moja kati ya mabao 7 dhidi ya Stoke.

Huko jijini London vijana wa Roy Hodgson imewachkua dakika 731 kufanikiwa kufunga bao lao la kwanza tangu kuanza kwa msimu, na kupata ushindi wao wa kwanza pia dhidi ya mabingwa watetezi Chelsea baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1. Mabao ya Crystal palace yamefungwa na Yohan Cabaye na Wilfried Zaha huku lile la Chelsea likifungwa na Tiemoue Bakayoko.

Wachezaji wa Crystal Palace wakishangilia Ushindi.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *