MAAJABU:Mchezaji wa Bolivia ahaha kupiga picha na timu ya taifa ya Brazil.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Bolivia Marcelo Moreno,ameiacha dunia na mshangao baada ya kujumuika na timu ya taifa la Brazil katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Marcelo Moreno ambaye baba yake mzazi ni raia wa Brazil amewahi kuitumikia timu ya taifa la Brazil katika ngazi za miaka chini ya 17 na 18 ambako alifanikiwa kushinda kiatu cha dhahabu.

Moreno akiwa na timu ya taifa ya vijana ya Brazil

Moreno anaecheza katika ligi ya nchini China, amewahi pia kuvichezea vilabu vya Flamengo na Cruzeiro vionavyoshiriki ligi kuu nchini Brazil katika nayakati tofauti tofauti.

alipoulizwa baada ya mchezo Moreno alisema

kwa muda mrefu nimekua nikitamani kupiga picha na timu ya Brazil, nilijaribu Novemba mwaka jana ikashindika, leo nimepata nafasi nimefanya hvyo. Kabla ya mchezo nilishazungumza na Neymar nahodha wa Brazil na tukalipanga vyema, nimefanikiwa na hii kumbukumbu ntaitunza milele

Marcelo Moreno akipambana na Neymar katika mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo huo uliochezwa nchini Bolivia ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *