MABADILIKO SIMBA: Jaji apewa jukumu la kusimamia zabuni

JAJI Mstaafu Thomas Mihayo ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya itakayosimamia masuala ya uuzaji na ununuzi wa hisa za klabu ya Simba kuelekea mabadiliko ya uendeshaji katika klabu hiyo.

Agosti 20 mwaka huu mkutano mkuu wa klabu hiyo ulipitisha mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo kwa njia ya hisa ambapo asilimia 50 atapewa mwekezaji mmoja, 10 zitachukuliwa na wanachama walio hai na 40 zinazobaki kuwa mtaji wa klabu.

 

Katibu mkuu wa klabu ya Simba, Dk Arnold Kashambe ametangaza kamati hiyo yenye wajumbe watano ambayo itaketi keshokutwa Jumatano kwa ajili ya kuanza mchakato huo mara moja.

Kamati hiyo itaongozwa na Jaji Mihayo pamoja wajumbe wanne ambao ni Damas Ndumbaro, Abdulrazak Badru, Azan Zungu na Yusuph Majid.

“Kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba imeunda kamati maalum kwa ajili ya kushughulia masuala ya zabuni kuelekea katika mfumo mpya wa uendeshaji kwa njia ya hisa, kamati hiyo itafanya kikao cha kwanza Jumatano wiki hii,” alisema Dk Kashambe.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *