MADRID KUVUNJA REKODI YA USAJILI KWA NEYMAR

Klabu ya Real Madrid ipo tayari kuvunja rekodi ya usajili kwa Neymar ili kumchukua katika majira ya joto ya mwaka 2019.

Mshambuliji huyo raia wa Brazil alisajiliwa na Paris Saint-Germain kwa dau lililovunja rekodi ya uhamisho ya pauni 200 milioni akitokea Barcelona mwaka jana ambapo Rais wa Madrid, Florentino Perez ameweka wazi anataka kumsajili nyota huyo.

Gazeti la Marca ambalo hutoa taarifa za ndani za Madrid limeripoti kuwa hata Neymar mwenyewe yupo tayari kujiunga na miamba hiyo.

Marca limeripoti kuwa ada ya Neymar itakuwa Euro 400 milioni sawa na pauni 356 milioni.

“Napenda kuwa na wachezaji bora klabuni kwangu na Neymar ni mmoja wao. Mlango upo wazi kwake kama anataka kujiunga nasi tunamkaribisha sana,” alisema Perez.

PSG ilimsajili Neymar ili kuwasaidia kushinda taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya hivyo hawatakuwa tayari kumuachia kabla ya kutimiza lengo hilo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *