MAHADHI ATUMIA DAKIKA MOJA KUIPA USHINDI YANGA

Winga Juma Mahadhi ameifungia bao pekee timu yake ya Yanga katika mchezo wa awali wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya St Louis kutoka visiwa vya Shelisheli akitumia dakika moja kufanya hivyo.

Mahadhi aliingia dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu na kufanikiwa kufunga bao hilo dakika moja baadae akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Geodfrey Mwashiuya.

Matokeo hayo yanaiweka Yanga kwenye mazingira magumu ya kufuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kuwa magumu zaidi kwa mabingwa hao.

Mshambuliji Obrey Chirwa alikosa mkwaju wa penati dakika ya 22 baada ya mlinzi Hassan Kessy kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.

Ibrahim Ajibu alipoteza nafasi ya wazi dakika ya 60 baada ya kupaisha mpira kufuatia kazi nzuri ya Chirwa.

Yanga itasafiri kuelekea Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika Februari 20.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *