MAJERAHA YAMFANYA MBARAKA KUWAKOSA ZANZIBAR

Mshambuliaji Mbaraka Yusuph wa Kili Stars anatarajiwa kukosa mchezo unaofuata dhidi za Zanzibar Heroes baada ya kupata majeraha katika mchezo wa jana dhidi ya Libya kwenye michuano ya Chalenji inayo endelea nchini Kenya.

Kili Stars na Zanzibar ambazo zote zipo kundi A zitakutana Alhamisi ya Disemba 7 katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kutokana na kuhusisha timu zinazojuana vizuri.

Mbaraka hakuweza kufanya mazoezi hii leo baada ya maumivu hayo ya msuli na atapumzishwa katika mchezo huo ili aweze kucheza dhidi ya Rwanda kwenye mchezo wa tatu.

Leo jioni Kocha wa Kili Ammy Ninje atakutana na wachezaji wake kuutathmini mchezo wa Libya ambao ulimalizika kwa sare ya bila kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos jana.

Kilimanjaro Stars ipo kundi A pamoja na timu za Zanzibar, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *