MAJIBU YA MOURINHO KUHUSU KAULI HII YA GUARDIOLA

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ameponda kauli ya Pep Guardiola kuwa atamkosa kiungo wake mchezeshaji David Silva katika mchezo wa ‘Manchester Derby’ utakaofanyika Old Trafford siku ya Jumapili

Guardiola amesema Silva yupo kwenye hati hati ya kukosa mchezo huo ambapo pia amemuengua kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa leo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk, lakini Mourinho anaamini hiyo ni ‘Mind game’.

“Unataka nikwambie ukweli au unataka nini? Ukweli ni kwamba Eric Bailly hatacheza lakini Phil Jones anaweza kucheza.

“Marouane Fellaini ana nafasi ya kucheza, Zlatan Ibrahimovic atacheza Nemanja Matic aliumia lakini atacheza lazima huo ni kweli. Michael Carrick hana nafasi ya kucheza.

“Lakini ulisikia kuwa Alexandre Lacazette kuwa hatacheza, leo David Silva unaambiwa kuwa nae hatocheza wote huo ni ukweli pia,” alisema Mourinho.

Mara zote kabla ya mchezo huo huwa na maneno kutoka kwenye kambi za timu zote.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *