MAJIMAJI YAJICHIMBIA NYASA KUIWINDA MBAO

Timu ya Majimaji itaondoka kesho Songea kuelekea wilaya ya Nyasa kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC utakaofanyika Novemba 18 kwenye uwanja wa Majimaji.

Majimaji itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja iliyopata Ijumaa iliyopita dhidi ya Stand United katika uwanja huo huo.

Msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Ndunguru amesema wachezaji walipewa mapumziko ya siku nne ambapo wameanza kurejea jana na leo ili kesho kuanza safari ya kuelekea Nyasa.

Kikosi cha Majimaji pamoja na benchi la ufundi litaondoka kesho kuelekea wilaya ya Nyasa ambapo kitacheza mechi mbili za kirafiki. Mchezo wa kwanza utakuwa Jumamosi dhidi ya Mbamba Bay na Jumapili tutacheza na Mkali Stars ili kuwaweka sawa wachezaji kabla ya kukutana na Mbao,” alisema Ndunguru.

Ndunguru amesema Mbao wamekuwa wazuri zaidi wakicheza kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuliko wakitoka kitu ambacho kinawapa matumaini ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Timu hizo zote zina pointi nane huku Mbao ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *