Majimaji yamalizana na ‘wanajeshi’ 20 kwa ajili ya VPL

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa, timu ya soka ya Majimaji imekamilisha usajili wa wachezaji 20 kwa mkataba wa mwaka mmoja kila mchezaji na bado wanaendelea kusaka wengine.

Msemaji wa Majimaji Nathan Mtega amesema ingawa timu hiyo imekumbwa na ukata wa kifedha wanajitahidi kwa hali na mali kusajili wachezaji wazuri ili kuleta ushindani wa kweli katika ligi kuu ya Vodacom.

Wachezaji waliosajiliwa ni pamoja na Jerson John Tegete (Mwadui), Tumba Lui Swed (Mbeya City), Marcel Bonaventure (Majimaji), Sixmund Mwasekaga (Lipuli), Dan Mrwanda Kagera (Sugar), Jafar Mohamed (Toto) pamoja na   Abdulhalim Humud.

Jerry Tegete, straika mpya wa Majimaji

Wengine ni Kenedy Kipepe (Majimaji),  Seleman Kasgir (Mwadui), Yakub Kibiga (Majimaji), Paul Maona (Majimaji), Hashim Musa (Majimaji), Alex Zegega Kondo (Majimaji), Seliha Ally Malenda (Africa Lyion), Peter Mapunda( Majimaji) Andrew Ntara (Prison), Mpoki Mwakinyuke (Majimaji) bila kusahau Sadiq Gawaza (Jkt Mlale).

Pia alisema wachezaji watakaofanya vizuri wataboreshewa mikataba yao kabla ya msimu kumalizika.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *