Malinzi Azipeleka Simba, Mbao kwa Waziri Mkuu

RAIS wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamali Malinzi ametangaza kuwa fainali ya kombe la FA kati ya Simba na Mbao FC itapigwa kwenye dimba la Jamhuri mjini Dodoma ziliko ofisi za Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa.

Akizungumza katika ufunguzi wa kozi ya awali ya makocha na waamuzi iliyoandaliwa na chama cha soka wilaya ya Ubungo, Malinzi alisema wameamua kuipeleka fainali hiyo Dodoma kwavile uwanja wa Taifa utakuwa katika matengenezo.

“Ukarabati wa uwanja wa Taifa utaanza Mei 21 na fainali ni Mei 28 kwahiyo ni wazi utakuwa haujakamilika ndio sababu tumeupeleka mchezo huo mjini Dodoma,” alisema Malinzi.

IMG-20170502-WA0018

Hata hivyo mapema jana Rais huyo kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter aliandika kuwa shirikisho hilo lingetangaza tarehe na muda wa kuchezeshwa droo ya kupata uwanja kwa ajili ya fainali hiyo ambayo ilipangwa kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Azam.

Simba imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Azam bao 1-0 ushindi unaofanana na ule walioupata Mbao dhidi ya mabingwa watetezi Yanga hapo juzi kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *