MAN CITY, CHELSEA KUZINDUA EPL LEO

Pazia la ligi kuu nchini Uingereza (EPL) litafunguliwa wikiendi ijayo ambapo leo kutakuwa na mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa katika uwanja wa Wembley saa 11 jioni kwa saa za nyumbani.

Man City ndio mabingwa wa ligi hiyo msimu uliopita huku Chelsea wakiwa mabingwa FA hivyo kukutana ili kuzindua ligi msimu wa 2018/19.

Chelsea ina kocha mpya Maurizio Sarri raia wa Italia aliyechukua mikoba ya Antonio Conte aliyetupiwa virago licha ya kuwapa taji la FA.

Timu zote hajifanya usajili mkubwa kipindi hiki cha usajili ambapo City ya Pep Guardiola imemuongeza Riyard Mahrez kutoka Leicester City huku Chelsea ikimsajili Joginho kutoka Napoli mlinda mlango Robert Green.

Hata hivyo Mahrez alipata maumivu ya mguu katika moja ya mechi za kujiandaa na msimu hivyo huenda asiwe sehemu ya kikosi cha City kitakachoshuka dimbani jioni ya leo.

Ligi hiyo itaanza rasmi Ijumaa ijayo kwa mchezo mmoja kati ya Manchester United dhidi ya Leicester City utakaopigwa katika uwanja wa Old Trafford saa 4 usiku.

Jumamosi Agosti 11 kutakuwa na mechi tisa lakini kivutio itakuwa ni kati ya Arsenal dhidi ya City utakaopigwa katika dimba la Emirates.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *