MAN CITY HII HAKUNA WA KUISIMAMISHA SPURS YAPIGWA 4G

Manchester City imeendelea kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuifunga Tottenham Hotspur mabao 4-1 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Etihad.

City imeshinda michezo 17 kati ya 18 ya ligi iliyocheza mpaka sasa ikiwa mbele kwa alama 14 dhidi ya wanashika nafasi ya pili Manchester United.

Moto uliowashwa na vijana hao wa kocha Pep Guardiola umeshindwa kuzuilika baada ya kutoka sare mchezo mmoja na kushinda mingine yote iliyocheza.

Mabao ya City yalifungwa na Ilkay Gundogan, Kelvin de Bruyne na Raheem Sterling aliyefunga mabao mawili wakati lile la kufutia machozi la Spurs likifungwa na Christian Eriksen.

City imefikisha pointi 52 huku ikionekana ni vigumu kuizuia isitwae taji hilo msimu huu wakati United yenye alama 38 itashuka kesho kucheza na West Bromwich.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *