Manchester City yaendeleza dozi Marekani

NASHIVILLE, Marekani
MANCHESTER City imeendelea kutoa dozi kubwa nchini Marekani kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham Hortspur katika mchezo wa kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

City imeonyesha kiwango safi katika mchezo huo hukuikishuhudiwa beki Kyle Walker akianza dhidi ya waajiri wake wa zamani.

Wiki iliyopita City iliifunga Real Madrid mabao 4-1 ambapo katika michezo miwili wamefunga jumla ya mabao saba huku wakiruhusu moja tu nyavuni kwao.

Wachezaji wa City wakishangilia moja ya mabao yao dhidi ya Spurs

Mabao ya City yalifungwa na John Stones, Raheem Sterling na Brahim Diaz ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kwenye kikosi cha kocha Pep Guardiola.

Kabla ya vipigo hivyo vizito ilivyotoa katika michezo miwili City ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa majirani zao Manchester United wiki mbili zilizopita katika mechi ya kirafiki.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *