MANZESE BINGWA NDONDO CUP

Timu ya Manzese United imeibuka bingwa wa michuano ya Sports Extra Ndondo Cup baada ya kuifunga Kivule FC bao moja katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Bandari.

Manzese na Kivule zote zimeshiriki michuano hiyo yenye kuvuta hisia za mashabiki wengi jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza na kufika hatua.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Seleman Shisha akijifunga kipindi cha kwanza ambalo lilidumu mpaka mtanange huo unamalizika.

Mshambuliaji Idd Seleman ‘Nado’ ameweka historia ya kuchukua ubingwa huo mara mbili akiwa na timu tofauti.

Mwaka jana alichukua ubingwa akiwa na Misosi FC na leo ametwaa tena akiwa na Manzese.

Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu TFF, Wallace Karia pamoja na Mwenyekiti wa chama soka Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo walihudhuria fainali hiyo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *