MASOUD: NAFURAHI KUONA WACHEZAJI WOTE WAKIWA FITI

Kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema anafarijika kuona wachezaji wote wa Wekundu hao wakiwa fiti na kufanya mazoezi ya pamoja.

Simba inajiandaa na mchezo wa ligi kesho dhidi ya Maafande wa Tanzania Prisons utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kocha Masoud amesema wachezaji waliokuwa majeruhi wote wamerejea uwanjani kitu ambacho kinawapa wigo mpana wa kupanga kikosi kulingana na mechi yenyewe.

“Kikosi kizima cha Simba kipo vizuri na kinafanya mazoezi pamoja wakati mwingine hata kama mchezaji hachezi lakini akiwa fiti anaweza kutumika muda wowote,” alisema Djuma.

Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 55 alama nane juu ya Yanga walio nafasi ya pili.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *