Matunda ya uwekezaji kwa Vijana, Azam yajivunia 6 “under 20”

Uongozi wa klabu ya Azam umetoa shukrani kwa shirikisho la Soka nchini TFF kwa kuwaamini vijana sita wanaonolewa katika shule ya mpira ya klabu hiyo watakaojiunga na timu ya taifa chini ya miaka 20.

Akizungumza na waandishi wa habar msemaji wa Klabu ya Azam Jafari Iddi, amesema kwao ni fahari kubwa sana na jambo la kujivunia kuona TFF imeona juhudi zilizowekwa na Azam katika soka la vijana na kuwaamini vijana kwenda kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

“Tunapenda kuishukuru TFF kwa kuchagua vijana sita kutoka timu ya vijana ya Azam watakaojiunga na kikosi cha taifa chini ya miaka 20, hii inaonesha ni jinsi gani mchango wetu unathaminiwa katika kuendeleza soka la vijana na pia mchango wa vijana hao kwa taifa letu,” alisema Jafari Iddi

wachezaji waliochaguliwa katika kikosi hiko wakitokea Azam ni pamoja na Peter Paulo aliefunga bao la kusawazisha katika mchezo wao uliopita dhidi ya Singida United, Mohammed Kijiko, Adathir Rajab, Saidi Issa, Oscar Masai na Ramadhan Mohamed.

Uwekezaji katika soka la vijana umekua ni moja ya ajenda inayozungumzwa zaidi katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania, lakini bado muamko wa vilabu katika uwekezaji huo umekua mdogo sana changamoto kubwa ikielezwa kuwa ni ukosekanaji wa fedha kwa vilabu vya Tanzania.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *