MAYANGA AELEZA SABABU YA KUMTUMIA HIMID, BEKI WA KULIA

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga amesema aliamua kumtumia nahodha Himid Mao nafasi ya beki ya kulia kwa sababu ya uzoefu na aina ya wapinzani wao Benin wanavyocheza.

Mayanga amesema kitaalamu Himid alipaswa kucheza nafasi ile ukilinganisha na wachezaji wengine waliokuwa kikosini baada ya kukosekana kwa beki Erasto Nyoni anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Kocha huyo wa zamani wa Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar amesema mara kadhaa hata klabu yake ya Azam imekuwa ikimtumia Himid kama beki wa kulia kwahiyo haikuwa mara yake ya kwanza.

“Baada ya kumkosa Erasto nikaamua kumpanga Himid beki wa kulia kutokana na uzoefu wake na alicheza vizuri pia tuliwaheshimu sana wapinzani wetu Benin,” alisema Mayanga.

Himid amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji jambo ambalo lilileta maswali miongoni mwa wadau wa soka nchini kutokana na kutozoeleka katika nafasi hiyo.

Baada ya kukosekana kwa Erasto wengi waliamini kuwa angewatumia kati ya Boniface Maganga au Nurdin Chona katika nafasi hiyo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *