MAYANGA AIBADILISHIA MFUMO BENIN, STARS YATOA SARE

Baada ya kocha Salum Mayanga wa taifa Stars kubadili mfumo wa kiuchezaji kipindi cha pili kwa kuruhusu timu kushambulia alifanikiwa kusawazisha bao katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha kwanza Stars ilicheza kwa kujilinda na kuwaruhusu wenyeji kutawala hasa sehemu ya kati lakini viungo Mudathir Yahaya na Hamis Abdallah walikuwa muhimili mkubwa kuilinda idara ya ulinzi.

Baada ya kurejea kutoka mapumziko Stars walirudi kwa nguvu na kulishambulia lango la Benin kwa kasi hali iliyozaa matunda katika dakika za mwanzo tu kipindi cha pili.

Mshambuliaji Elius Maguri alifunga bao hilo dakika ya 50 baada ya kupokea pasi ndani ya 18 iliyopigwa na Shiza Kichuya.

Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati lililofungwa na nahodha Stephen Sessegnon dakika ya 30 baada ya mchezaji wa Benin kuushika mpira nje ya 18 bila mwamuzi kufahamu.

Katika mchezo huo nahodha Himid Mao alianza kucheza kama beki wa kulia badala ya kiungo mkabaji hali iliyompa shida huku wenyeji wakitumia zaidi upande huo katika kupandisha mashambulizi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *