Mbao Yatia Doa Sherehe za Ubingwa Yanga

MBAO FC imetia doa sherehe za ubingwa wa Yanga kufuatia kuwafunga mabingwa hao watetezi bao moja katika mchezo wa mwisho wa kuhitimisha ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Huo unakuwa ubingwa wa 27 kwa Yanga huku wakiutwaa kwa mara ya tatu mfululizo na kuweka historia nzuri katika ligi kuu Tanzania bara.

IMG-20170520-WA0046

kikosi cha Yanga kikishangilia baada ya kutawazwa Mabingwa wa VPL 16/17

Bao pekee la Habib Hajji dakika ya 23 liliiwezesha Mbao kusalia ligi kuu kufuatia kufikisha pointi 33.

Simon Msuva ameibuka mfungaji bora wa ligi baada ya kufunga mabao 14 ambapo msimu uliopita mshambuliaji Amissi Tambwe alikuwa kinara kwa kufunga mabao 20.

Huu ni mwanzo mzuri kwa kocha George Lwandamina ambaye aliichukua timu hiyo katikati ya msimu kutoka kwa Mholanzi Hans Van Pluijm ambaye nae alitwaa mara mbili mfululizo.

Yanga imemaliza ligi ikiwa na pointi 68 sawa na Simba lakini uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa umeiwezesha kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *