MBEYA CITY YAFUATA UBANI TANGA WA KUIA YANGA JUMAPILI

Timu ya Mbeya City imeweka kambi ya muda jijini Tanga kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaofanyika kwenye uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili.

Wagonga nyundo hao waliingia jana jijini humo ambapo leo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union inayoshiriki ligi daraja la kwanza kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa moja ya maandalizi ya mchezo huo.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Shah Mjanja amesema kikosi chao kipo kamili kwa ajili ya mechi ya Jumapili huku wachezaji Erick Kyaruzi na John Kabanda ambao walikuwa majeruhi hali zao zikiwa zinaendelea vizuri.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na tupo jijini Tanga na leo tutacheza na Coastal mechi ya kirafiki ikiwa ni kujiweka sawa kabla ya kukutana na Yanga mwishoni mwajuma.

“Hali za wachezaji wetu Kyaruzi na Kabanda wanaendelea vizuri kuna uwezekano mkubwa wa kuwatumia kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga,” alisema Shah.

Msemaji huyo alisema kuhusu suala la usajili wataangalia mapendekezo ya mwalimu yanataka nini kabla ya kufanya maamuzi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *