Messi hatihati, Harrry Kane “kama Kawa”,Brazil waomba Msaada wa Oxygen Bolivia….Mambo kadhaa yaliyokupita kufuzu kombe la dunia.

TIMU ya taifa ya England imefanikiwa kufuzu kushiriki kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi mwakani baada ya mshambuliaji wake Harry Kane kufunga bao la ushindi dakika za lala salama dhidi ya timu ya taifa ya Slovenia mchezo uliopigwa katika dimba la Wembley.

Harry Kane akifunga bao pekee lililoipeleka Engalnd kombe la dunia 2018 Urusi.

Huko jijini Buenos Aires nchini Argentina, timu ya taifa la Argentina iko mguu nje mguu ndani kushiriki kombe la dunia mwakani, baada ya kukubali sare ya bila ya kufungana dhidi ya Peru.Argentina iliyosheheni nyota duniani wakiwemo Dyabala, Messi , Di maria na wenzao wengi wanashikilia nafasi ya 6 wakifikisha alama 25 katika michezo 17 huku wakisalia na mchezo mmoja tu dhidi ya Ecuador utakaochezwa juma lijalo.Timu 4 zinazoshika nafasi ya juu barani Amerika kusini hufuzu moja kwa moja na ile ya 5 kulazimika kucheza mchezo wa mtoano dhidi ya New Zealand.

Nyota wa Argentina wakitoka uwanjani vichwa chini baada ya mchezo dhidi ya Peru.

Huko nchini Bolivia, timu ya taifa la Brazil imeshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Bolivia.Wachezaji wa Brazil ilibidi wapate msaada wa mashine za Oxygen kwa ajili ya upumuaji kutokana na umbali mkubwa wa mita 3,637 kutoka usawa wa bahari unaosababisha hali ya upumuaji kuwa ngumu kwa wageni wa eneo hilo.Brazil tayar imeshafuzu kombe la dunia kwa kufikisha alama 38 kwenye michezo 17 na kuongoza kundi hilo.

Neymar akiwa amelala kiwanjani huku akiwa haamini nafasi ya goli aliyokosa.

KUPATA MATOKEO YA MICHEZO YOTE.

Bonyeza hapa kupata matokeo ya mechi zote

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *