MESSI KUMALIZA SOKA LAKE KATIKA TIMU HII

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amesema bado ana matumaini kuchezea timu yake ya utotoni ya Newell’s Old Boys kabla ya kuamua kustaafu soka.

Taarifa zinasema kuwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Argentina mustakabali wake ndani ya Barcelona utajulikana mwezi Januari kufuatia mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Barcelona, Oscar Grau alisema klabu hiyo itampa mkataba wa maisha mwezi uliopita baada ya kukubali kuongeza miaka minne lakini Messi 30 mpaka sasa bado hajasaini.

Messi aliiacha Newell’s kuelekea Nou Camp akiwa na miaka 13 lakini kwa sasa ameweka wazi kuwa angependa kurejea katika mji aliozaliwa wa Rosario kumaliza soka lake.

“Dhamira yangu ni kucheza timu ya Newell’s, nilikuwa na ndoto hiyo tangu nikiwa mtoto. Nikienda kwenye klabu hii huwa najihisi kama nacheza ligi ya Hispania ila hakuna anayejua kitu gani kitatokea miaka michache ijayo,” alisema Messi.

Messi pia amesema asingependa nchi yake kupangwa kundi moja na nchi za Hispania kwenye hatua za makundi ya kombe la dunia mwakani huku akisema Brazil, Ujerumani na Ufaransa ndiyo timu anazozipenda kwenye michuano hiyo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *