Messi na maajabu yake, “Hat-trick” ya 44 yaipeleka Argentina kombe la dunia.

MESSI, linaweza kua ndio jina lilitajwa mara nyingi midomoni mwa wapenda soka duniani kuanzia jana jioni mpaka asubuhi ya leo, katika uwanja ulioko umbali wa juu sana kutoka usawa wa bahari, nyota huyo alifanikiwa kufunga mabao 3 yaliyoipeleka Argentina moja kwa moja kwenye fainali za kombe la dunia nchini Urusi.

Romario, mshambulia wa Ecuaor alianza kwa kuifungia nchi yake bao katika dakika ya 1 tu tangu kuanza kwa mchezo kabla ya Mesi kusawasisha na kuongeza mabao mengine 2 kufanya matokeo ya mwisho kua 1-3.

Mshambuliaji wa Ecuador,Romario akifunga bao la kuongoza dhidi ya Argentina.
Moja ya magoli aliyofunga Messi, na kufufua matuamini ya Argentina

Argentina iliingia katika mchezo huo ikiwa katika hatihati ya kutoshiriki kombe la dunia, ikihitaji zaid ushindi na kuomba matokeo mabaya kwa chile dhidi ya Brazil au Peru dhidi ya Colombia.Vijana hao wanaonolewa na Sampaoli walifanikiwa kutuliza vichwa vyao na kufanya kile ambacho wa Argentina wote walikua wakiomba kitokee katika mchezo huo.

Wachezaji wa Argentina wakishangilia kufuzu kombe la dunia.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *