Mexime na Wenzake Wamaliza Kozi ya Ukocha

KOZI ya ukocha wa daraja A inayotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) iliyokuwa ya siku 19 imefungwa leo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF Khalid Abdallah.

Kozi hiyo imejumuisha makocha 19 akiwemo Mecky Maxime ambao wamehitimu mafunzo hayo wakiungana na wengine 22 waliohitimu katika kozi iliyopita.

Akifunga kozi hiyo Khalid amewataka wahitimu hao kutoweka vyeti vyao kwenye makabati badala yake wanapaswa kuvitumia kwa ajili ya maendeleo ya soka la nchi hii kwakua ndiyo lengo lake.

“Mafunzo mliyopata mkayatumie vizuri kwa ajili ya maendeleo ya soka na sio kukaa na vyeti kwenye makabati itakuwa haijasaidia chochote,” alisema Khalid.

Kwa upande wake Meck Mexime ambaye ni mmoja wa wahitimu hao alisema mafunzo hayo atayafanyia kazi ipasavyo kwa ajili ya mafanikio ya timu yake ya Kagera Sugar.

“Namshuru Mungu nimemaliza kozi salama na nina amini mafunzo haya nitayatumia vizuri kwa ajili ya maendeleo ya timu yangu ya Kagera ambayo nipo nayo kwa sasa,” alisema Meck.

Wahitimu wote walipewa mipira mitatu kila mmoja na koni kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa vitendo katika mahali waendako.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *