MGHANA WA AZAM AAMUA KUVUNJA MKATABA

Mshambuliaji wa Azam FC, Bernard Arthur raia wa Ghana ameamua kuvunja mkataba kutokana na mambo kutomuendea sawa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao wa 442 wa Ghana.

Arthur ambaye ametokea klabu ya Liberty Professional ya Ghana amechukua uamuzi huo baada ya kushindwa kupata nafasi kubwa ya kucheza dimbani.

Licha ya kuwa na mwanzo mzuri Arthur ameshindwa kumshawishi kocha Aristica Cioba huku ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na kuondolewa na Mkurugenzi Mtendaji Abdul Mohammed.

Baada ya Abdul kufukuzwa kocha Cioaba alishindwa kumpa nafasi kitu kilichopelekea kushusha kiwango chake na kuamua kuvunja mkataba.

Arthur, 21 amefunga mabao sita katika mechi zake tano za mwanzo kabla ya kukumbwa na ukame wa mabao kitu ambacho kimemfanya atupwe benchi.

Ili kulinda kipaji chake Arthur ameamua kuvunja mkataba ili kutafuta timu ambayo itampa nafasi kubwa ya kucheza.

Kabla ya kujiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili Bernard alikuwa mfungaji bora wa Liberty msimu uliopita.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *