MKHITARYAN: ‘NAINJOI’ KUCHEZA NA AUBAMEYANG

Nyota mpya wa Arsenal, Henrikh Mkhitaryan amekiri kuwa anafurahia kucheza pamoja na mshambuliji Pierre Aubameyang baada ya kuwasaidia Washika bunduki hao kushinda mabao 3-0 dhidi ya Watford.

Kiungo huyo alisema ilikuwa ngumu kushinda mchezo wa jana kutokana na kupoteza mechi tatu zilizopita kabla ya kukutana na Watford.

Raia huyo wa Armenia amesema siku zote anafurahi kucheza na Aubameyang tangu wakiwa Borussia Dortmund kabla ya kukutana tena Arsenal kwakua anavitu maalum uwanjani.

“Nadhani imekuwa ni ndoto kukutana tena baada ya kuachana Dortmund, nina furaha kwa hilo.

“Namfahamu vizuri Aubameyang, ni mmoja wa marafiki zangu wa karibu, nina furaha kumuona akiwa amevaa jezi ya Arsenal pamoja na mimi. Napenda kucheza pamoja nae,” alisema Mkhitaryan.

Katika mchezo wa jana Mkhitaryan na Aubemayang walifunga kila mmoja bao huku wakitengezeana mabao hayo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *