Mkutano mkuu Simba uko pale pale

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Kisutu imetupilia mbali zuio la mkutano mkuu wa klabu ya Simba uliopangwa kufanyika keshokutwa Jumapili, Agosti 13.

Jana Baraza la wadhamini likiongozwa na katibu wake Mzee Hamis Kilomoni lilienda Mahakamani hapo kuzuia kutofanyika kwa mkutano huo kwa sababu viongozi wakuu wa klabu hiyo wanashikiliwa na vyombo vya dola.

Rais wa klabu hiyo Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ wanashikiliwa na vyombo vya dola mwezi mmoja na nusu sasa kutokana na kutuhumiwa kwa kosa la utakatishaji fedha ambapo kesi yao imetajwa mara kadhaa mahakamani hapo.

Miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni mabadiliko ya katiba ambayo yakifanyika yatamwezesha mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘MO’ kuwekeza klabuni hapo.

Suala la uwekezaji ndani ya klabu hiyo limewagawanya wanachama ambapo kuna baadhi wanakubali wengine wanapinga.

Uongozi uliopo madarakani umekuwa ukitoa elimu ya uwekezaji kwa wanachama wa klabu hiyo kupitia matawi tangu walipotangaza tarehe ya mkutano huo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *