MKWASA AKANUSHA KUJIUZULU YANGA

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa amekanusha taarifa kuwa amejiuzulu nafasi yake baada ya kutuhumiwa kuhusika na kuondoka kwa kocha mkuu George Lwandamina.

Mchana wa leo kulikuwa na taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa Mkwasa ameamua kujiweka pembeni baada ya kunyooshewa vidole kila timu inaposhindwa kupata matokeo.

Wiki iliyopita Lwandamina alitangazwa kuwa kocha mpya wa Zesco United ya Zambia huku akisema moja ya sababu iliyomfanya kuondoka ni katibu huyo kutomtimizia mahitaji yake.

Mkwasa amesema taarifa za yeye kujiuzulu Yanga sio za kweli ni upotoshaji wa hali ya juu ili kuleta taharuki miongoni mwa wapenzi na wanachama wa klabu hiyo.

“Mimi bado ni Katibu mkuu wa klabu ya Yanga, taarifa za kujiuzulu ni uzushi mtupu ili kutuchanganya tushindwe kufanya mambo yetu,” alisema Mkwasa.

Mkwasa ameongeza kuwa kikosi cha Yanga kitaondoka kesho asubuhi kuelekea nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha utakaofanyika Aprili 17.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *