Mlioanza Usajili Someni Taarifa ya TFF

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kufungua dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa ligi 2017/18.

TFF imetoa taarifa hiyo ikiwa tayari baadhi ya klabu zimeanza kufanya usajili wake hasa kwa wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao.

PicsArt_06-09-11.19.30

“Dirisha hilo linafunguliwa Juni 15, na litafungwa Agosti 6, mwaka huu hivyo kila timu inayoshiriki michuano iliyotajwa hapo juu, inaarifiwa kufuata kalenda hiyo ambayo tunaitangaza sasa,” ilieleza taarifa hiyo.

TFF imetoa tahadhari kwa klabu zote kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu ambazo hazitakamilisha usajili kama ilivyotokea msimu uliopita kwa baadhi ya timu kushindwa kufanya usajili kwa wakati hadi dirisha lilipofungwa.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *