MLIPILI,MWASHIUYA, MHILU WAITWA TIMU YA TAIFA U23

Nyota Yusuph Mlipili wa Simba Geofrey Mwashiuya, Yusuph Mhilu na Emmanuel Martin wa Yanga wamejumuishwa kwenye kikosi cha awali chenye wachezaji 35 wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 kinacho jiandaa na michuano ya Olimpiki jijini Tokyo, Japan.

Mlipili ambaye ametokea Toto African ya Mwanza bado hajapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Joseph Omog sawa na Mhilu kwa upande wa Yanga lakini wanategemewa kuwa na mchango mkubwa kutokana na uzoefu walionao.

Kikosi hicho kitakuwa na kambi ya siku 10 ambapo wachezaji hao 35 watachujwa na kubaki 25 watakaounda timu ya taifa kwa umri huo.

Kocha mkuu wa timu hiyo Oscar Mirambo amesema wanatarajia kupata mchezo miwili ya kujipima nguvu na timu zinazo shiriki ligi kuu ili kuwapa kipimo nyota hao.

Kikosi kitakuwa na wachezaji 35 ambao tutawachuja kupata 25 ambao ndio itakuwa timu ya taifa ya chini miaka 23 itakayo shiriki kufuzu michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo mwaka 2020,” alisema Mirambo.

Wachezaji waalioitwa na Mirambo ni Metacha Mnata, Joseph Prosper, Masoud Abdallah, Yahaya Zayd, Abbas Kapombe (Azam), Mwashiuya, Mhilu, Martin, Cleotas Sospeter (Yanga), Eliud Ambokire, Emmanuel Kakuti, Medson Mwakatunde (Mbeya City), Ismail Aidan, Salum Kihimbwa, Hassan Mganga (Mtibwa Sugar).

Wengine ni Omari Mponda, Ayoub Masoud, Baraka Majogoro (Ndanda), Stanley Angeso, Adam Salamba (Stand United), Yusuph Kagoma, Salum Chuku (Singida United), Paul Lyungu, Idrisa Mohammed (Majimaji), Liza Mwafwea, Bakari Kijuji (Prison), Mlipili (Simba), Joseph Ilunda(Jkt Ruvu), William Patrick (Ruvu Shooting).

Derushi Shaliboko (Ashanti), Awesu Ally (Mwadui), Award Salum, Agaton Mapunda (Njombe), Mohammed Habib (Miembeni) na Feisal Abdallah (JKU).

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *