MNYAMA AZIDI KUNGURUMA AIPIGA NNE GENDARMERIE

Timu ya Simba imeanza vema michuano ya awali ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga mabao 4-0 Gendarmerie Nationale ya Djibouti mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa.

John Bocco akimtoka beki wa Gendarmerie
Nahodha wa timu hiyo John Bocco alifunga mabao mawili kati ya hayo yote kwa kichwa dakika za 32 na 45.

Kiungo Said Ndemla alifunga bao la kwanza dakika ya kwanza kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni.

Simba ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo ambao walikuwa na uwezo wa kupata mabao zaidi ya hayo huku Gendarmerie ikicheza kwa kujilinda zaidi.

Emmanuel Okwi alifunga bao la nne dakika za nyongeza kipindi cha pili nje ya 18 baada ya kutengewa mpira.

Mchezo wa marudiano utafanyika nchini Djibouti Februari 21 mwaka huu.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *