MNYAMA YUKO FULL MZIKI KUIKABILI MWADUI ALHAMISI

Kikosi cha timu ya Simba kimewasili jijini Mwanza asubuhi ya leo kikiwa vizuri kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC utakaofanyika kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 4-0 iliyopata katika mchezo wa awali wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Djibouti mwishoni mwa juma lililopita.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Masoud Djuma amesema wachezaji wako kwenye hali nzuri na morali iko juu tayari kwa mchezo huo.

Masoud ameiambia Simba Makini kuwa mlinzi Asante Kwasi ndiye atakosekana kutokana na kuwa na kadi tatu za njano huku wengine wakiwa fiti.

“Tumewasili salama mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui, wachezaji wako vizuri kwa mechi.

“Kwasi tumemuacha Dar es Salaam sababu ana kadi tatu za njano hivyo akitumikia adhabu hiyo,” alisema kocha Masoud.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *