MO ENERGY YAIMWAGIA SIMBA MAMILIONI

Klabu ya Simba imeingia mkataba wa udhamini na kampuni ya A1 production inayozalisha vinywaji vya MO Energy wenye thamani ya Shilingi milioni 250.

MO Energy wanakuwa wadhamini wenza katika klabu ya Simba baada ya wadhamini wakuu kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa.

Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewaambia Waandishi wa habari kuwa kiasi hicho cha pesa katika mkataba wa MO Energy kitatumika katika ujenzi wa uwanja wao wa Bunju.

Try Again ameongeza kuwa bado wapo na kwenye mazungumzo na wadhamini mbalimbali kuendelea kufanya nao na kazi kwakua uendeshaji wa klabu unahitaji pesa nyingi na dhamira yao ni kuifanya Simba kuwa timu bora ya kisasa.

“Simba tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya MO Energy wenye thamani ya sh milioni 250 ambapo wataonekana katika vifaa vyetu mbalimbali vya klabu ya Simba,” alisema Try Again.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MO Energy, Mwanasala Soud amesema wanaamini watapata faida ya udhamini kwakua Simba ni brand kubwa.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *