Moro Kids yatishia kufunga kituo kisa Simba

UONGOZI wa kituo cha kulea na kuendeleza vipaji vya soka cha Moro Youth & Women Soccer Development Center maarufu kama Moro Kids cha mjini Morogoro umetishia kukifunga kituo hicho kwa maelezo kuwa hawapati faida yoyote.

Moro Kids wamelalamika kuwa klabu ya Simba imekuwa ikishindwa kutimiza makubaliano yao pale inapowasajili wachezaji kutoka kituoni hapo au kutokea Mtibwa ambako wengi hupitia huko kabla ya kuonekana na timu za ligi kuu.

Timu ya vijana ya Moro Kids ilipotwaa ubingwa wa Airtel Rising Stars

Katika barua yake kwa katibu mkuu wa TFF, mratibu wa kituo hicho Rajabu Kidangule amesema anakusudia kumshauri mkurugenzi wa kituo Profesa Madundo wakifunge kutokana na dharau anazoonyeshwa na viongozi wa Simba pindi anapofuatilia haki zao.

Hata hivyo katika barua hiyo ambayo ameambatanisha baadhi ya mikataba, Kidangule amekiri kufanya makubaliano kadhaa na Simba kwa mdomo bila kuandikishiana popote.

Wachezaji wanaotajwa katika malalamiko hayo ni pamoja na Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Shomari Kapombe, Ally Shomari, Salim Mbonde na wengine ambao hawapo Simba kwa sasa kama Edward Christopher na Hassan Kessy.

Hizi hapa ni kurasa za barua hiyo;

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *