Mourinho Jeuri, Kuwapumzisha Nyota Wote Dhidi ya Arsenal

VIGO GARCIA, Hispania
MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amesema atawapumzisha baadhi ya wachezaji katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Emirates.

United iliibuka na ushindi wa bao dhidi Celta Vigo katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya pili ya Europa jana, ushindi wa kwanza katika michezo 10 tangu Aprili mosi.

Kutokana na vijana wa Mourinho kuwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi nchini Uingereza, michuano ya Europa ndio inabaki kuwa nafasi pekee waliyonayo ya kufuzu michuano ya klabu bingwa kwa msimu ujao.

“Wachezaji waliocheza dakika nyingi hawatacheza Jumapili dhidi ya Arsenal,” alisema Mourinho.

Mpira wa adhabu wa Marcus Rashford uliipa United ushindi nchini Hispania wakiwa kwa bao hilo la ugenini na kuwaweka kwenye mazingira mazuri katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Old Trafford Alhamisi ijayo.

2017-04-16T164622Z_135362782_MT1ACI14779832_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-CHE-800x504

Kikosi cha United kilipata msaada baada ya kurejea kwa beki Chris Smalling ambaye alikuwa nje ya uwanja tangu mwezi Machi kutokana na maumivu ya goti.

Eric Bailly alikuwa na maumivu ya enka na kiungo Paul Pogba alikuwa akisumbuliwa na misuli ambao wote walianza katika mchezo huo.

Rashford alifanyiwa mabadiliko ambapo Mourinho alisema ni kutokana na kupata maumivu katika mchezo huo.

“Anafanya kazi kila siku, katika klabu pamoja na timu ya taifa. Anapenda kujituma.

“Wakati mwingine anabaki peke yake uwanjani kujifunza kupiga mipira ya adhabu.

“Lilikuwa ni bao zuri. Mpira ulikimbia haraka sana na mlinda mlango alifanya jitihada lakini ilikuwa ngumu kudhibiti,” Mourinho alimwagia sifa kinda huyo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *