MOURINHO KUVUNJA BENKI KWA NYOTA HUYU WA REAL MADRID

Kocha Jose Mourinho yupo tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa katika majira ya joto mwakani kwa ajili ya nyota wa Real Madrid Marco Asensio ili kuimarisha kikosi chake.

Jarida la Don Balon la Hispania limeandika kuwa United ipo tayari kutoa ofa kubwa kwa ajili ya kunasa saini ya kiungo huyo.

United inajiandaa kuvunja benki kutoa uero 200 milioni sawa na pauni 177 milioni ili kumpata Mhispaniola huyo.

Mourinho anataka kumpa mkataba wa miaka mitano ambapo atavuna kiasi cha pauni 24 milioni kwa mwaka ili kumtoa Santiago Bernabeu.

Mreno huyo anataka kujenga kikosi kitachokuwa na uwezo wa kutwaa ligi ya mabingwa barani Ulaya akiamini Asensio ambaye mkataba wake ni Real unamalizika mwaka 2023 kuwa anafiti katika mpango wake.

Kocha Zinedine Zidane mara kadhaa amekuwa amkitumia Asensio kutokea benchi lakini bado ana uwezo mkubwa wa kufunga.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *