Mpira utakaotumika kombe la dunia huu hapa.

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Adidas, imezindua rasmi aina ya mpira utakaotumika katika fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwakani.

Telstar18, ndio jina la mpira huo, ikiwa ni muendelezo wa mpira aina ya Telstar unaotimiza miaka 48 tangu ulipotumika kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia mwaka 1970 nchini Mexico.

Mpira aina ya Telstar baada ya kuboreshwa.

Adidas imeuboresha zaidi mpira huo kwa teklnolojia ya kisasa itakayouwezesha kuunganishwa na mitambo ya kidigitali, na unatajwa kuwa ndio aina ya kwanza ya mpira kutumika ukiwa na nakshi za rangi nyeupe na nyeusi kuanzia miaka ya 1970.

Mpira aina ya Telstar uliotumika mwaka 1970 nchini mexico.
.

Kwa mara ya mwisho aina hii ya mipira ilitumika katika kombe la dunia mwaka 1974 Ujerumani Magharibi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *