MSENEGAL, MMALI WATUA SIMBA

NA MWANDISHI WETU,

manara

WASHAMBULIAJI Pape Abdoulaye Ndaw wa Senegal na Makan Dembele wa Mali, ni wachezaji walio kwenye mipango ya kufanya majaribio na kikosi cha Simba.

Uongozi wa timu hiyo leo mchana ulimshusha Ndaw kwa majaribio, huku kesho wakitarajiwa kumpokea Dembele.

Habari za ndani kutoka kwa mmoja wa viongozi wa timu hiyo ilisema kuwa mchezaji Dembele anatarajiwa kuwasili kesho na moja kwa moja atakwenda Visiwani Zanzibar kuungana na wachezaji wengine kwa ajili ya kambi na majaribio yake.

Kiongozi huyo alisema mchezaji huyo pamoja na Ndaw watajaribiwa katika michezo yao ya kirafiki miwili ambayo watacheza wakiwa visiwani humo kabla ya kurejea jijini hapa.

Chanzo hicho kilisema kati ya Ndaw na Dembele, atakayeonyesha kiwango ndio watamsajili baada ya kuridhishwa na kiwango chao ambacho kocha mkuu Dylan Kerr, ndio atatoa majibu.

“Kuna watu wanabeza hizi harakazi zetu, lakini nataka kuwaambia Simba imepanga kufanya vizuri msimu ujao ndio maana tunajaribu kutafuta kilicho bora zaidi na sio ili mradi bora” kilisema chanzo hicho.

Katika hatua nyingine kikosi hicho leo saa 9 Alasiri, kinatarajiwa kuondoka jijini hapa na kurejea Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu soka Tanzania Septemba 12.

Wachezaji wote waliosajiliwa na kikosi hicho wamekwenda visiwani humo isipokuwa baadhi ya wachezaji waliopo kambini Uturuki na kikosi cha timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’.

 

Simba wanatarajiwa kufungua pazia la mchezo wa ligi kuu kwa kukwaana na timu ya African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *