MSIMTIMUE KLOPP ATAMALIZA TOP 4 MSIMU HUU

Nyota wa zamani wa Liverpool Graeme Souness amesema ‘Majogoo’ wa Anfield wanapaswa kuendelea kumuamini kocha wao Jurgen Klopp na anaweza kumaliza katika nafasi nne za juu msimu huu.

Liverpool ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingireza wakishinda mchezo mmoja katika mechi sita zilizopita.

Kibarua cha Klopp kipo shakani kwani wapo nyuma kwa alama 12 dhidi ya vinara Manchester City ambapo Souness amesema ana matumaini kuwa timu yake hiyo ya zamani itamaliza nafasi nne za juu.

Liverpool wanapaswa kubaki na Klopp, anafaa kuendelea kuwepo Anfield, ni mtu mwenye mizuka aliyevaa moyo wa Liverpool.Nadhani klabu inatakiwa kuendelea kumpa muda zaidi,” alisema Souness .

Graeme James Souness.

Liverpool walikubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Tottenham Hotspur jumapili iliyopita baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Maribor kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katikati mwa juma lililopita.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *