Mtibwa Yaanza Usajili kwa Kunasa Nyota Wawili

KLABU ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imefanikiwa kunasa saini za nyota wawili kwa ajili kuimarisha kikosi chake kwa cha msimu ujao wa ligi 2017/18.

Nyota hao waliosajiliwa ni mshambuliaji kutoka katika timu ya Polisi Morogoro Salum Ramadhani ‘Chuji’ na beki wa kati Hussein Idd kutoka JKT Oljoro.

Salum Ramadhani ‘Chuji’ 

Mtandao rasmi wa klabu hiyo umeandika nyota hao wameingia mkataba wa miaka miwili kila mmoja huku kocha wao Zuber Katwila  akishirikiana na benchi la ufundi amesema watapandisha baadhi ya nyota kutoka katika timu yao ya vijana.

Taarifa hiyo inasema Uongozi wa Mtibwa  unaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi ambapo usajili bado unaendelea na nyota wengine wanatarajiwa kujiunga kwa Wakata Miwa hao siku chache zijazo.

Wakat huo huo uongozi wa klabu hiyo umetangaza kuwa mikataba ya wachezaji Jaffary Salum, Said Mkopi, Maulid Gole ‘Adebayor’, Said Bahanuzi, Vicent Barnabas, Ally Lundenga na Ally Shomary imekwisha.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *