MTIBWA YAITISHIA NYAU SIMBA

Timu ya Mtibwa Sugar imejinasibu kuisambaratisha Simba kwa kuishushia kipigo katika mchezo wa ngao ya jamii wa kufungua pazia la ligi utakaopigwa Agosti 18 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mtibwa imerejea Manungu Turiani ikijiandaa na mchezo huo baada ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika fukwe za Coco Beach wiki kadhaa zilizopita.

Msemaji wa Wakata miwa hao, Thobias Kifaru amesema licha ya kuwa licha ya Simba kuweka nchini Uturuki lakini hawatishiki na watawafundisha adabu siku hiyo Kirumba.

Kifaru ameongeza kuwa hawatishwi na usajili uliofanywa na Simba msimu huu huku pia akikimwagia sifa kikosi chao ambacho kinaundwa na wachezaji wazawa kuonyesha cheche katika ligi msimu huu.

“Tunawasubiri Simba warudi kutoka Uturuki tukutane CCM Kirumba tuwafundishe jinsi ya kusakata kabumbu katika mchezo wa ngao ya jamii,” alisema Kifaru.

Mtibwa itaiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho kutokana na kutwaa ubingwa wa FA huku Simba ikiwakilisha kwenye ligi ya mabingwa Afrika.

Mchezo wa ngao ya jamii huashiria ufunguzi wa ligi kuu bara ambayo msimu huu wa 2018/19 utashirikisha timu 20 badala ya 16 kama ilivyokuwa awali.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *