MUDATHIR: BADO TUNA NAFASI YA KUTWAA TAJI LA VPL

Licha ya kutoka sare ya tatu mfululizo nahodha msaidizi wa timu ya Singida United, Mudathir Yahya anaamini kuwa bado wana nafasi ya kutwaa taji la ligi kuu msimu huu.

Singida inayonolewa na kocha Hans Van Pluijm ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 14 baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Yanga kwenye uwanja wa Namfua jioni ya leo.

Kiungo huyo wa zamani wa Azam FC amesema matokeo wanayopata hayawakatishi tamaa na wataendelea kupambana mpaka mwisho ili watwae ubingwa.

Bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa, ligi ni ngumu ila tutaendelea kupambana mpaka mwisho kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema Mudathir.

Mudathir amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Pluijm kutokana na kiwango bora alicho onyesha tangu kuanza kwa msimu huu.

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga amemuongeza kiungo huyo kwenye kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Benin Novemba 12.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *