Mwarami Kocha Mpya wa Makipa Simba

KLABU ya Simba imemtangaza Mwarami Mohammed kuwa kocha wa makipa ambapo kuanzia msimu ujao ataanza kuonekana katika benchi la ufundi la Wekundu hao.

Ujio wa Mwarami ndani ya Simba unahitimisha zama za kocha Idd Salum ambaye alijiunga na Wekundu hao mwaka jana na kufanikiwa kuvaa medali kwa kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho.

Mtandao maalum wa klabu hiyo umeandika ujio wa kocha huyo ikionyesha ni mwanzo wa mabadiliko katika benchi la ufundi huku taarifa zikisema kocha msaidizi Jackson Mayanja hatokuwepo kikosini hapo msimu ujao.

Simba imeanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi leo katika uwanja wa Chuo cha Polisi uliopo Kurasini huku wachezaji wachache wakijitokeza katika siku hii ya kwanza ya mazoezi hayo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *