MZAMIRU,NYONI ‘OUT’ STARS, MKUDE, MUDATHIR ‘IN’

Nyota wawili wa timu ya Simba Mzamiru Yassin na Erasto Nyoni wameenguliwa kwenye kikosi cha Stars kinacho jiwinda na mchezo wa kirafiki wa ugenini dhidi ya Benin wiki ijayo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Wachezaji hao walionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mwezi uliopita.

Uamuzi huo umetokana na maelekezo kutoka Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kuwa nyota hao wanapaswa kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

Viungo Jonas Mkude anayechezea Simba pia na Mudathir Yahaya wa Singida United wameitwa kuchukua nafasi za wachezaji hao.

Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema wamepokea maelekezo kutoka FIFA na kumwambia kocha wa timu ya Taifa, Salum Mayanga ambaye alifanya mabadiliko kidogo kikosini.

Wachezaji Mzamiru na Nyoni wameondolewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinacho jiandaa na mchezo wa Kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin kufuatia kadi nyekundu walizopata katika mechi na Malawi mwezi uliopita.Kocha Mayanga amewaongeza kikosini Mkude na Mudathir kuchukua nafasi za wachezaji hao,” alisema Lucas.

Stars itaingia kambini Jumapili Novemba 5 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika nchini Benin Novemba 12.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *