NAHODHA STARS, AWAPIGA MKWARA KINA SAMATTA

NA MWANDISHI WETU, Dar

mecky4

NAHODHA na beki wa kati wa kikosi cha timu ya soka taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameitazama safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayoongozwa na Mbwana Samatta na kuwataka waongeze umakini katika eneo la 18 ya wapinzani.

Kikosi hicho jana kimelazimidshwa sare ya bila kufungana na timu ya Nigeria, huku washambuliaji wake wakishidwa kuzitumia nafasi.

Akizungumza na Simba Makini, marab baada ya mchezo huo kumalizika Cannavaro alisema, safu ya viungo ya Stars ilitengeneza nafasi za kufunga, lakini ukosefu umakini kwa wachezaji wa safu ya ushambuliaji ndio uliowanyima ushindi katika mchezo huo.

Cannavaro alisema, ni muda sasa wa safu hiyo kujipanga vyema kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Chad.

“Siwezi kuwataja majina ni wachezaji gani ambao wamefanya tukose ushindi, mimi ni nahodha na kila mtu ameona kilichofanywa na washambuliaji wetu.

“Huu ni muda wao kukaa chini na kutafakari jinsi ya kuweza kutumia nafasi chache zinazoweza kupatikana ndani ya mchezo ili tupate ushindi kwenye mchezo mwingine unaofuata.

“Kikosi kilicheza vizuri muda mwingi wa mchezo, lakini ukosefu umakini kwa watu wa mbele ndio uliofanya tusipate mabao” alisema Cannavaro.

Hata hivyo nahodha huyo aliwasifu wapinzani Nigeria na kusema walicheza vizuri.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *